Erik akiondoka,Sancho Anarejea United

Winga Jadon Sancho ambaye ni mali ya Manchester United anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Borussia Dortmund atakuwa tayari kuanza tena maisha mapya ya soka ndani ya klabu ya Manchester United na iwapo meneja Erik ten Hag ataondoka.

Sancho hana mahusiano mazuri na Meneja wa Manchester United Ten Hag na kabla ya kutolea kwa mkopo walikuwa na migogoro kadhaa na kukosekana kwa muafaka baina yao hali iliyopelekea kwa nyakati tofauti mchezaji huyo kuondolewa katika kikosi cha kwanza na kutolewa katika Kundi la Watsapp la klabu hiyo baada ya Sancho kumsgutumu kocha wake kuwa ni muongo Mnamo mwezi Septemba mwaka jana baada ya

Mholanzi huyo alijibu kwa kumfukuza Sancho kwenye kikosi cha kwanza, huku mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 73 kutoka Dortmund akilazimika kufanya mazoezi na wachezaji wa akademi ya Manchester United.

Jadon Sancho hajakata tamaa katika maisha yake ya soka ya Manchester United na yupo tayari kurejea ndani ya klabu hiyo endapo tu kocha Erik Ten Hag ataondoka msimu huu wa joto na nafasi ya mchezaji huyo ni kubwa kutokana na meneja wa ufundi anayetarajiwa kujiunga na United Jason Wilcox anayetarajiwa kumpa Sancho nafasi nyingine ndani ya klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *