Rais Samia Ziarani Uturuki

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X,Waziri wa mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Uturuki kunzia hii leo April 17 hadi April 20,2024.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha na kukuza uhusiano baina ya nchi hizi mbili na Tanzania inatarajia kusaini mikataba nane kama sehemu ya kuimarisha biashara ambapo pia kupitia ziara hiyo Rais Dkt.Samia anatarajia kukutana na viongozi wa wafanyabiashara wa Kituruki 100 kwa nia ya kuwahamasisha kufanya uwekezaji nchini.

Makamba amesema pia makubaliano ya pande mbili yatakayofanyika kupitia ziara hiyo yataangazia maeneo mbalimbali ikiwemo Elimu ya Juu,Ubunifu na Teknolojia ambapo pia Rais Samia anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake,Rais wa Uturuki Recep Tayyip Edorgan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba akiwa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *