DKT. BITEKO ASHIRIKI MKUTANO WA NISHATI WA MAWAZIRI EAPP

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo 17 Aprili, 2025 ameshiriki Mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Nishati wa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki ambao ni wanachama wa Umoja wa Soko la pamoja la Kuuziana Umeme na Kuimarisha Mifumo ya Gridi ya EAPP (Eastern Africa Power Pool).

Mkutano huo wa siku 2 umeanza Aprili 16, 2025 na unatarajiwa kumalizika leo Aprili 17, 2025 jijini Kampala nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *