CHADEMA YAJIONDOA RASMI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi – INEC Ramadhani Kailima amesema Chama cha Demokrasia na maendeleo – CHADEMA hakitashiriki Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025 na chaguzi zote ndogo kwa muda wa miaka mitano kufuatia kutosaini kanuni za Maadili ya Uchaguzi.

Kailima amsema hayo mara baada ya zoezi la kusini kanuni za maadili ya Uchaguzi leo April 12, 2025 katika ofisi za Tume hiyo Njedengwa jijini Dodoma ambapo vyama vya siasa 18 ndivyo vimesaini isipokuwa CHADEMA.

“Chama cha Chadema ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” Ramadhan Kailima mkurugenzi wa Tume huru ya Uchaguzi – INEC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *