Burna Boy atishia kuacha muziki

Staa wa Afrobeats Burna Boy ametishia kuja kuacha mambo ya muziki, kwa kile kinachotokana cha maslahi kuwa finyu.

Hivi karibuni staa huyo amenukuliwa akisema , anaumizwa na takwimu zilizopo za mapato kwake kwani zimekuwa ndogo sana kwa muda mrefu hivyo anafikiria miaka ijayo anaweza kuacha muziki au kusimama kimuziki na kisha kurejea kwa kishindo kama Rihhana.

Majarida ya Marekani ambayo yanafuatilia kwa ukaribu shughuli za wasanii wa Kiafrika, Burna Boy aliwahi nukuliwa akilalama kuwa japo anafanya vizuri lakini kiasi cha fedha ambacho anakipata kutokana na kazi zake ikiwemo ya usambazwaji wa miziki wake kimekuwa ni cha kiwango cha duni.

Mwaka wa 2022 kuelekea mwaka huu wa 2023 Burna Boty aliingiza zaidi ya dola milioni 300 lakini ilielezwa kwamba katika kipindi cha miaka 3 mfululizo, utajiri wake haujawahi kuongezeka hata kwa asilimia moja na umekuwa hivyo hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *