
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, Tundu Antipas Lissu ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, nafasi ambayo kwa muda mrefu imekua ikishikiliwa na Freeman Mbowe.
Lissu ametoa taarifa hiyo rasmi, wakati akizungumza na Waandishi wa habari siku ya Alhamisi Desemba 12, 2024 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.