Google imetoa list ya Watu na vipengele mbalimbali vya maudhui vilivyotafutwa zaidi katika mtandao huo kwa mwaka 2024 ambapo Rais mteule wa sasa wa Marekani, Donald Trump na Msanii mkongwe wa Hip hop Marekani P. Diddy wameongoza kwa kutafutwa zaidi kwa mwaka 2024.
Katika mwaka wa 2024 Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameongoza orodha ya Watu waliotafutwa zaidi katika mtandao huo, ukitoa Trump wengine ni Binti Mfalme wa Wales, Catherine, Kamala Harris, Imane Khelif.
Kwenye list ya Wasanii waliotafutwa zaidi katika Google 2024, Msanii mkongwe ‘Diddy’ Combs ameongoza orodha hiyo kwa kutafutwa zaidi akifuatiwa na mkali wa RnB, Usher Raymond, Linkin Park, Sabrina Carpenter, Justin Timberlake, Angela Aguilar, Drake, Tracy Champman.
Contact Us
P. O. BOX 71, Shinyanga, Tanzania
+255 766 408 253
info@jambofm.co.tz