Bima na NMB Bank Imetiki Kahama

Benki ya NMB imezindua kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga,Kanda ya Magharibi kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kukata Bima ili kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto, mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusababisha kuyumba kiuchumi.

Uzinduzi huo uliokwenda sanjari na utoaji elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kukata Bima umefanyika leo Jumamosi Aprili 20,2024 katika Kituo cha Mabasi cha CDT Mjini Kahama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema lengo la Kampeni ya Umebima ni kutoa elimu ya masuala ya bima, kutoa ushauri pamoja na kuuza bima mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.

Akiwa viwanja vya CDT – Kahama leo Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema hakuwa na budi kuzindua kampeni ya umeBIMA na NMB Kahama kwa sababu ya uchangamfu wa mji huo na wepesi wa watu wake kupokea na kufanyia jambo, pia amesema kampeni hii itatapakaa mikoa mingi kama Simiyu, Tabora, Kigoma, Geita na Katavi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *