Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Asilimia 30 Pekee Ya Ardhi nchini Imepimwa Vijijini

Na Costantine James,Geita

Imeelezwa kuwa upimaji wa ardhi katika vijiji hapa nchini bado ni changamoto kubwa inayopelekea vijiji vingi kushindwa kupimwa hasa katika halmashauri za wilaya ambapo mpaka sasa asilimia 30 pekee ya vijiji vyote Tanzania vimepimwa hali inayopelekea kuendelea kushamiri kwa ujenzi holela kila kukicha katika maeneo mbalimbali ambayo hayajapimwa hadi sasa.

Hayo yamebainishwa leo Juni 13, 2024 na Mkurugenzi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Usimamizi na Uratibu (NLIPC) Kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Jonas Masingija wakati wa uwasilishaji wa rasimu ya mpango wa matumizi ya ardhi wa halmashauri ya wilaya bukombe Mkoani Geita amesema Tanzania ina Vijiji 12318 lakini asilimia 30 tu vimepimwa huku kati ya halmashauri za wilaya 139 halmashuri 48 pekee zimefanya mpango wa matumizi ya ardhi katika baadhi ya vijiji.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mkuu wa Wilaya Bukombe Paskasi Muragili amesema ujio wa rasimu ya mpango wa matumizi ya ardhi katika wilaya hiyo utatoa dira sahihi juu ya matumizi mazuri ya ardhi na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo.

Nao baadhi ya wadau wa ardhi pamoja na wananchi wa wilaya ya Bukombe walioshiriki katika kikao hicho wakaomba mpango huo wa matumizi ya ardhi uzingatie zaidi katika kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji ili kumaliza changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo mara nyingi inasababishwa na mwingiliano kati wakulima na wafugaji katika maeneo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *