Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa imemtia hatiani Dickson Mbwilo (42) Mkazi wa Kitelewasi na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumlawiti mke wake.
Kulingana na maelezo ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka (32), mumewe alikuwa akimfanyia kitendo hicho pale anapokuwa amekosea ili iwe ndiyo adhabu yake hali ambayo ilimsababishia sehemu zake za siri kuharibika vibaya.
Hata hivyo, mpaka kufikia hatua ya Mbwilo kutiwa hatiani na kufungwa, mlalamikaji hakuwahi kufika kortini kutoa ushahidi wake, isipokuwa Mahakama iliamua kuegemea maelezo yake aliyokuwa ameyaandika Polisi.