Omben amchinja mke wake na kutenganisha kichwa na kiwiliwili

Mwanaume mmoja aitwaye Omben Kilawa mkazi wa kijiji hicho wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya anatuhumiwa kumuua mke wake Happness Mwinuka kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na Kiwiliwili.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Machi 13, 2024 ambapo jirani wa familia hiyo amesema alisikia kelele kama watu wanagombana lakini baada ya nusu saa kukawa kimya na kuamua kupiga yowe ndipo watu walipojitokeza na polisi walipofika walibomoa mlango wa chumbani kwao na baada ya kuingia Kilawa alikuwa ameshatekeleza mauaji kwa kumchinja mke wake na kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *