Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Afrika Kusini kutengeneza mipira ya kuzuia maambukizi ya VVU

Kampuni moja nchini Afrika Kusini imesema itaanza hivi karibuni kutengeneza mipira maalum ya kondom ya kuwalinda wanawake kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Kampuni ya afya ya Kiara iliyopo mjini Johannesburg itaanza kutengeneza vifaa hivyo miaka ijayo na inakadiria kutengeneza hadi kinga milioni 1 kwa mwaka.

Hadi sasa kinga hiyo iliyotengenezwa mfano wa pete, karibu 500 zinapatikana kwa sasa kote barani Afrika na hutolewa bure kwa wanawake. Aina hiyo ya kinga inayowekwa sehemu ya siri ya mwanamke, husambaza dawa inayozuia maambukizi ya VVU na tayari zimeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani WHO na katika nchi karibu kumi na mbili.

Kulingana na takwimu ya WHO, Virusi vya Ukimwi bado ni sababu kuu ya vifo kwa wanawake barani Afrika na asilimia 60 ya maambukizi mapya hutookea kwa wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *