Kampuni ya Delta Air Lines imesema itatoa Dola 30,000 kwa kila abiria aliyekuwemo ndani ya ndege iliyopata ajali wakati ikitokea Minneapolis Nchini Marekani na kupinduka wakati ikijaribu kutua jijini Toronto Nchini Canada.
Katika taarifa iliyotolewa na Shirika hilo, ilieleza kuwa wote abiria wote isipokuwa mmoja walikuwa wameruhusiwa kutoka kwa huduma ya matibabu hadi kufikia Jumatano asubuhi ya Februari 19, 2025.

Akielezea chanzo cha ajali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Deborah Flint alisema uwanja wa ndege ulipokea kiwango kisicho cha kawaida cha theluji siku chache kabla ya ajali hiyo.
Alisema, “kulikuwa na zaidi ya inchi 20, sentimeta 50 za theluji iliyokusanyika, na ucheleweshaji na ughairi mwingi wa maamuzi katika sehemu hii ya Canada na U.S. Kaskazini-mashariki, ulisababisha ajali.”