Halmashauri 41 Pekee zimetenga fedha kwa ajili ya Ununuzi Ww Mafuta ya Watu wenye Ualbino.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Festo Dugange amesema hadi sasa ni halmashauri 41 pekee nchini zilizotenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya watu wenye Ualbino, hivyo Serikali itaweka kipaumbele zaidi kwa mwaka wa fedha ujao kuhakikisha fedha hizo zinaendelea kutengwa.

Dugange Alikuwa akijibu swali Bungeni jijini Dodoma la Mbunge Stella Ikupa aliyetaka kufahamu ni hatua gani zimechukuliwa kwa halmashauri zisizonunua mafuta ya watu wenye Ualbino.

Naibu Waziri Dugange amesema Serikali inaendelea kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika uwekezaji wa mazao mbalimbali ambayo yatazalisha mafuta hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *