
Simba SC imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 kwa usawa wa mabao 1-1 katika mechi mbili za robo fainali dhidi ya Wydad.
Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca nchini Morocco, Simba haikuwa na mabadiliko katika kikosi chake kilichoanza mechi ya Dar na iliruhusu bao dakika ya 24 likifungwa na Bouly Sambou kwa kichwa lililosalia hadi dakika 90 (1-0).
Simba iliziba njia za Wydad kwa muda mwingi licha ya makosa machache waliyofanya ambayo wapinzani hawakutumia vizuri.