Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO: Nilianza na Duka la reja reja -Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Group

Wafanyabiashara nchini wametakiwa kutumia fursa zilizopo na kuwa wabunifu katika kutafuta na kuibua miradi pamoja na kuwa na nidhamu katika utekelezaji wa miradi ili iweze kuwa endelevu.


Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Jambo Group of Companies Bw.Salum Khamis Salum Januari 11,2024 wakati akizungumza mara baada ya kupokea ugeni kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) na kutumia fursa hiyo kuishukuru serikali na TIC kwa mchango wake katika ustawi wa uwekezaji nchini.

Watu wengi hushindwa kufanya maamuzi ya uthubutu wa kufanya uwekezaji kutokana na kuwa na hofu mablimbali ikiwa ni pamoja na kufikiria kwamba kuna ugumu katika kufanya hivyo.


Ili kuhakikisha unaweza kuanza Fresh katika kile ulichodhamiria kuwekeza hapa nchini,Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Jambo Group Of Companies Bw.Salum Khamis Salum kupitia video hii ameelezaea uzoefu alioupitia katika uwekezaji hadi pale alipofikia hivi sasa na kuwezaesha upatikanaji wa ajira kwa watu zaidi ya watu 16400.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *