Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Sitaruhusu Mahakama kukwamisha miradi yangu

Rais wa Kenya William Ruto ameapa kutongoja idhini ya Mahakama ili kutekeleza ajenda yake ya kimaendeleo kwa mujibu wa manifesto ya Kenya Kwanza, akitangaza vita kwa maafisa wa idara hiyo ambao amedai hupokea rushwa kwa ajili ya kutoa ilani za kukwamisha maendeleo.

Rais Ruto ameyasema hayo akiwa katika Kaunti ya Nyandarua huku akiwajia juu maafisa wa mahakama ambao amesema kazi yao ni kusimamisha miradi kupitia ilani za mahakama.

“Ninaheshimu uhuru wa mahakama, lakini kile sitakubali na naapa kukisimamisha ni utundu, ukiritimba na ufisadi wa wachache ndani ya idara hiyo kwa kuwa walio na uwezo kwa mujibu wa katiba ni wananchi wenyewe,” akasema Rais Ruto.

Rais wa Kenya amesema kuwa ajenda yake imetekwa nyara na “mitandao ya ufisadi iliyoenea hadi mahakamani ambako kuna wachache washirika wa kuhongwa ili wakwamishe yale ya kuwafaa Wakenya kwa masilahi ya wachache”.

Matamshi hayo ya rais William Ruto wa Kenya yamekemewa vikali na aliyekuwa rais wa Muungano wa Mawakili nchini Kenya (LSK) Bw Okong’o Omogeni huku mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa ushuru wa ujenzi nyumba tarehe 14 mwezi huu wa Januari.

Okong’o Omogeni ameitaka Idara ya Mahakama isitishike na matamshi hayo na kumkumbusha Rais Ruto kwamba yuko chini ya taasisi kadha ikiwemo mahakama na kwamba kujaribu kukaidi mfumo wa kisheria ni kukaribisha mtafaruku mkubwa nchin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *