Klabu ya Namungo Fc kupitia mtandao wake wa kijamii wamemshukuru na kumtakia kila la kheri aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Denis Kitambi katika majukumu yake ya ukocha sehemu nyingine nje na klabu hiyo.

Namungo wapo nafasi sita (6) wamecheza michezo 13 wameshinda michezo minne (4) wakapata sare michezo mitano (5) na wamepoteza michezo minne (4) wamekusanya jumla ya alama 17.
Michezo yao sita (6) ya mwisho wameshinda mechi tatu (3), sare michezo miwili (2) na kupoteza mchezo mmoja (1) kwa ufupi tu kati ya hiyo michezo 6 sawa na alama 18 wamevuna alama 11 wakapoteza alama 7.