Aliyekuwa Katekista wa Kanisa Katoliki Makambako, Daniel Philipo Mwelango (43) amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji.
Daniel alitenda tukio hilo Februari 8, 2022 kwa kumuua Daniel Elias Myamba (43) ambapo alifanya maandalizi kwa kuandaa Panga, Chuma na Mifuko ya kuzuia Damu isisambae na mingine ya kuhifadhi Mwili wa marehemu.
Mshtakiwa alimuua Daniel aliyekuwa Katibu wa Halmashauri ya Walei kwa kumpiga na chuma kwenye Kisogo, alipofariki akamkata vipande viwili na kuvipakia katika Mifuko, akashindwa kuubeba Mwili, akaamua kutoroka kuelekea Dar es Salaam.