VIDEO: Mtu mmoja asombwa na maji baada ya kupata ajali

Mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Lembe Salimu Makenze Mwenye Umri wa Miaka 27 amefariki dunia kwa kusombwa na Maji baada ya kupata ajali kwenye daraja mpakani mwa Kayenze na izunya wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita na kusombwa na Maji.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita Grace Kingalame amesema tukio hilo limetokea Disemba 11 Majira ya asubuhi ambapo watu wawili dereva pikipiki maarufu kama Bodaboda waliokuwa wakisafiri kutoka Karumwa kwenda kafita wilayani humo walipata ajali wakati wakitaka kuvuka daraja ndipo waliposombwa na maji na kupelekea mama huyo kufariki dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *