Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watu 13 wakamatwa Zanzibar kwa unyanyasaji

Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kwa tuhuma za kuhusishwa kufanya vitendo vya udhalilishaji kwa watoto watatu Zanzibar.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Richard Mchomvu amesema jeshi la Polisi limefanya operesheni kufatia video iliyokuwa ikitembea kupitia vyombo vya habari watoto wakieleza kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na hivyo kuwahoji watoto hao na kutoa orodha ya watendaji wa makosa hayo.

Aidha Kamanda Mchomvu amekana kuwepo kwa mtandao rasmi wa wafanyaji wa matukio hayo, huku akieleza kuwa matukio hayo huchangiwa na kuporomoka kwa maadili ya watoto hao kwa kukosa malezi ya wazazi wawili.

Aidha amesema hadi sasa uchunguzi unaendelea na kesi tatu tayari zinaanza kusikilizwa mahakamani huku nyengine zikiendelea kufanyiwa uchunguzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *