Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanaoziba meno waongezeka

Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wametakiwa kuhakikisha wanasimamia matibabu bora ya Kinywa na Meno na kupunguza kung’oa meno bali waongeze watu wanaotibiwa meno.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo leo Novemba 22, 2023 wakati akifungua Kongamano la 38 la kisayansi la Kitaifa na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno linalofanyika Jijini Tanga.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Takwimu za kuziba meno zimeongezeka kutoka asilimia 2 mwaka 2020 mpaka asilimia 36.1 mwaka 2023 ambapo hali hii imetokana na uwekezaji wa Serikali ya awamu Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema, Takwimu za Mwaka 2022/2023 zinaonesha kuwa watu 541,159 waliooza meno yao ambapo watu 174,749 sawa na 32.3% walizibwa meno yao na watu 323,419 sawa na 59.8% waling’olewa meno yao.

Pia, Waziri Ummy amesema katika jitihada za Serikali za kuendelea kufanya mapinduzi Katika Sekta ya Afya imeweza kuajiri wataalam wa Kinywa na Meno 186 na kununua vifaa tiba vya kinywa na meno ikiwemo viti vya kutibia 55 vilivyokwenda kwenye Halmashauri 40 katika Mikoa yote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *