Saba wafariki 22 wajeruhiwa

Watu saba wamefariki na wengine 22 wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea katika Kijiji cha Kiwawa kilichopo Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, ikihusisha basi aina ya Scania mali ya kampuni ya Saibaba na basi aina ya Tata, mali ya kampuni ya Baharia.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Pili Mande amesema ajali hiyo imetokea Octoba 2 2023 jioni ambapo miongoni mwa waliofariki dunia ni pamoja na dereva aliyekuwa akiendesha basi la kampuni ya Saibaba, Lucas John (59) ambaye ni mkazi wa Arusha pamoja na dereva wa basi la kampuni ya Baharia, Omari Alli Abdalah (49) mkazi wa Dare s salaam.

Amesema miili ya marehemu watano bado haijatambuliwa majina yao mpaka sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *