Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

TASAF yanufaisha Kaya maskini 15,105

Jumla ya kaya masikini 15,105 mkoani Shinyanga ambazo ni sawa na asilimia 34.13 wamefaidika na mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF kwa kuanzisha miradi ya kilimo ufugaji na ujasiliamali na kaya 13000 kati ya hizo wamejiunga na mpango wa bima ya afya ya mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa ( ICHF) huku ikielezwa kuwa Hayo ni mafaniko makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kusaidia watanzania wasio na uwezo.

Takwimu hizo zimetolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme huku akiweka wazi kuwa mkoa wa Shinyanga umepokea zaidi ya shilingi bilioni 21 katika kutekeleza mpango huo kwa kipindi cha mwezi February 2021 mpaka June 2023 na kati ya fedha hizo zaidi shilingi bilioni 18 zilitumika kama malipo kwa walengwa na zilizosalia zilitumika kwa ajili usimamizi wa mpango na uendeshaji wa shughuli.

Baadhi ya wanufaika wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini wameishukuru serikali kwa kuwasaidia kwani hapo awali walikuwa na maisha magumu kutokana na hali ya umasikini hivyo kupitia mpango huo kwa sasa wanaendesha maisha yao ikiwa ni pamoja na kupata mitaji ya kufanya biashara ndogobndogo.

Mpango wa kunusuru kaya masikini unatekelezwabkatika kipindi cha pili cha TASAF awamu ya tatu kuanzia mwaka 2020 hadi 2023 na unatekelezwa katika mamlaka za utekelezaji 187, ambazo ni halmashauri zote za Tanzania bara na visiwani ikijumuisha vijiji/mitaa/shehia zote nchini na walengwa wa mpango huu kwa nchi nzima ni kaya zaidi ya 140,000 zenye watu wanaokadiriwakuwafikia 7,000,000 lengo likiwa kuongeza fursa za kipato kwa walengwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *