Rangi za suti muhimu kwa wanaume

Mambo vipi mwanamaisha fresh!!, leo naongea na wakaka jamani hasa kwenye sula la kutupia suti.

Najua wanaume wengi ni waoga wa rangi ila nataka kukupa rangi nne (4) ambazo mwanaume unatakiwa kuanza kuzifikiria kuwa nazo kwa sasa kwa kipindi hiki 2023.

Rangi ya suti, nyeupe au cream

Rangi hii inampendeza mtu yoyote na wa umbo lolote, ila kumbuka haiihitaji vitu vingi sana uvalie, kuanzia shati yake ya ndani hadi viatu. Hakikisha unatupia vitu vilivyo simple na vizuri, epuka kuchanganya na rangi hasa zile za kuwaka sana.

Rangi ya suti ya Kijani

Hii itabamba zaidi ukivalia shati nyeupe ndani na viatu vyeusi. Rangi ya kijani imekuwa miongoni mwa rangi pendwa kwa mwaka huu. Hapa utachagua kijani iliyoiva au illiyopauka. Pia kama unasaa valia ya brown/kahawia.

Rangi ya tatu: suti za burgundy

Rangi hii ni kama rangi ya damu ya mzee iliyopauka, wanaume si hampendi rangi nyingi basi hii pia inawafaa, hapa utavalia na shati ya pink mpauko, viatu vyako vikiwa brown, saa ya brown basi wee ukitokea watakutolea macho. Hii unaweza kuvaa hata kwenye harusi, kazini na hata mitoko ya kuvutia kama chakula cha usiku.

Rangi ya nne: suti ya brwon

Hii bhana inakubali na kila rangi ya shati kuanzia nyeupe, nyeusi, cream, ila viatu we vaa hata raba  tu utapendeza.

Rangi hii inamkubali mtu wa rangi zote na hii ukivaa watu wanaona huyu jaama ni noma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *