Staa wa muziki Akon, ametoa maujanja kama unandoto ya kuwa tajiri mkubwa na kusema kama unataka kuwa Tajiri basi kuwa bahili na yeye ndiye “mtu bahili zaidi duniani” kwa sababu lazima mtu awe mchoyo ili kuendela kuwa tajiri.
Kipitia podcat ya Impulsive, msanii huyo anafunguka” Ukitaka kubaki na utajiri basi kuwa bahili, na mimi ni mwanaume bahili Duniani, huwa nawaambia mwatu wangu na mashabiki usimiliki vitu vya gharama kama hauwezi kuvilinda, mfano nilijaribu kumiliki ndege, lakini ilidumu kwa miezi 6 tu; Niliuza kitu hicho haraka sana, kumiliki ndege inamaanisha unatumia dola milioni mbili hadi tatu kwa mwaka kwa ajili ya matengenezo. Unatumia zaidi kwenye matengenezo kuliko gharama halisi ya ndege.”