Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Cheni ya Rema yasababisha maafa Ethiophia

Kanisa la Othodoksi la Tewahedo la Ethiopia limeripotiwa kushinikiza wasimamizi wa Hoteli ya Sheraton mjini Addis Ababa kufuta tamasha la msanii wa muziki wa afrobeat kutoka Nigeria, Rema linalodaiwa kufanyika leo Septemba 9, 2023.

Mtu mmoja aliyeomba asitajwe jina lake amesema tamasha hilo lilikatishwa na wasimamizi wa hoteli baada ya viongozi wa Kanisa la Othodoksi “wenye nguvu” nchini humo kumshutumu mwimbaji huyo kuwa muumini wa shetani kutokana
mchoro uliotumika kwa tamasha hilo, ukimuonyesha Rema alivalia mkufu uliokuwa na kanisa linalowaka moto na misalaba iliyogeuzwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *