Ni Mtu mmoja pekee Vishwash Kumar Ramesh (40), raia wa Uingereza mwenye aliyenusurika katika ajali mbaya ya ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner, iliyoruka wakati ikiacha ardhi ya Ahmedabad, Nchini India.
Ndege hiyo iliyokuwa ikielekea jijiji London Nchini Uingereza, ilikuwa na abiria 242 na Wafanyakazi huku Ramesh akiwa ameketi katika kiti namba 11A, karibu na mlango wa dharura ya kutokea wa Ndege hiyo.

Ramesh amepata majeraha kifuani, machoni na miguuni, lakini alifanikiwa kutoka akiwa hai na katika mahojiano Hospitalini alipolazwa, alielezea namna ajali hiyo ilivyotokea.
Anasema, “sekunde thelathini baada ya kupaa, kulikuwa na kelele kubwa na kisha ndege ikaanguka. Yote yalitokea haraka sana. Nilipoinuka, kulikuwa na miili ikinizunguka.”

Hata hivyo, Mamlaka bado zinachunguza chanzo cha ajali hiyo, huku wataalamu wakihisi ni huenda ilitokea baada ya kushindwa kwa msukumo wa injini.
Kila binadamu mwenye kutambua uzito wa tukio hili suna shaka atakuwa anamshukuru Mwenye enzi MUNGU kwa uhai wa Ramesh na kumuomba azilaze roho za marehemu peponi na kuwapa faraja wafiwa.
