Wizara ya Maliasili na Utalii imetunga Kanuni za Usimamizi wa Shughuli za Uvuvi katika maeneo ya Hifadhi za wanyamapori (Mapori ya Akiba na Tengefu).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ambapo amesema tangazo hilo zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Namba. 781 la mwaka 2024.
Amesema, “Kanuni za Biashara za Nyara zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 884 la mwaka 2024, na Kanuni za Utalii wa Picha zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 875 la mwaka 2024. Vilevile, Wizara imefanya mapitio ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 780 la mwaka 2024 na Kanuni za Usimamizi wa Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) za mwaka 2018.

“Sambamba na hilo, Wizara imeandaa Mipango ya Jumla ya Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori (General Management Plan) ya Jumuiya za ISAWIMA (Kaliua), Ifinga (Madaba), Uyumbu (Urambo), na UKUTU (Morogoro). Katika hatua nyingine, Wizara imeandaa Mwongozo wa upatikanaji wa mazao ya wanyamapori na mimea inayosimamiwa na Mkataba wa CITES ili kuimarisha utekelezaji wa mkataba huo”. Amesema Dkt. Chana
Amesema Kanuni hizi zinalenga kuimarisha
uhifadhi shirikishi na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori.
“katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu, Wizara imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Utatuzi wa Migongano kati ya Binadamu na Wanyamapori”, amesema
“Katika kutekeleza Mkakati huo, Wizara kupitia TAWA, TANAPA na TAWIRI imekamilisha ujenzi wa vizimba 12 vya kudhibiti mamba na viboko katika Halmashauri za Wilaya za Bunda (3),
Korogwe (1), Ludewa (2), Uvinza (2), Tandahimba (2), Nanyumbu (1) na Mkinga (1)”. Amesema Dkt. Chana
Hata hivyo amesema, ujenzi wa vizimba sita
(6) unaendelea katika Wilaya za Buchosa (2), Sengerema (1), Bunda (1), Newala (1) na Kibiti (1). Vizimba hivyo vitasaidia kuimarisha usalama wa wananchi wanaotumia maji ya mito na maziwa katika maeneo hayo.