Simba SC, imethibitisha kuwa mchezo wake
wa mkondo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Mei 25, 2025 utafanyika katika uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kama ilivyoamriwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Mei 19, 2025 na Afisa Mtendaji Mkuu Klabu hiyo, Zubeda Sakuru imeeleza kuwa licha ya jitihada zote zilizofanywa na Serikali, TFF
na Simba ili kufanikisha mchezo huo ufanyike Uwanja wa Benjamin Mkapa, bado imeshindikana.
