NAIBU KATIBU MKUU WA CHADEMA ASHIKILIWA NA POLISI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mnamo tarehe 13 Mei 2025 majira ya saa 6:45 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi Kanda maalum hii leo Mei 13, 2025 imeeleza kuwa siku ya Jumanne, Golugwa alikamatwa akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels, Ubelgiji, kupitia lango namba 03 (Terminal 3) la uwanja huo wa ndege.

Imearifiwa kuwa, kukamatwa kwa kiongozi huyo wa juu wa chama cha upinzani kulitokana na “taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa Nchini.”

Kwasasa, uchunguzi wa kina unaendelea ukishirikisha Vyombo vingine vya Usalama, huku Polisi wakiahidi kutoa taarifa zaidi kadri hatua zitakavyopigwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *