GOMBATI AWATAKA WADAU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KUJA NA MKAKATI UNAOTEKELEZEKA

Na Frank Aman – Geita.

Wadau wanao fuatulia na kuchukua hatua za kupambana na Vitendo vya Rushwa Nchini wametakiwa kuja na Mikakati inayotekelezeka ili kuweza kugundua na kubainisha maeneo yanayominya haki kwa Wananchi na kuongeza madhara mengine yanayotia doa Nchi kwa ujumla kutokana na kuendelea kuwepo na Vitendo vya Rushwa hususani Mahala pa Kazi.

Akizungumza katika Warsha ya Wadau kuhusu Uzuiaji Rushwa Mahala pa Kazi na maeneo mengine iligoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati amesema kuendelea kwa Vitendo vya Rushwa Nchini inapunguza kasi Maendeleo ya maeneo mengi na pia kupunguza kasi ya ukuaji wa Biashara kwa eneo husika ambavyo Vitendo vya Rushwa vimekithiri.

Amesema Rushwa ni janga kubwa linalondelea kuathiri upatikanaji wa haki na Huduma muhimu za Kijamii ambapo kupitia Kongamano Hilo litawawezesha kujadili na kuweka Mikakati ya kuimarisha jitihada za kupambana na Rushwa.

Amesema kupitia Mkutano huo wenye Kauli Mbinu ya ‘Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu, Tutimize Wajibu Wetu’ ambao umewakutanisha Wadau kutoka Taasisi mbali mbali ikiwemo za umma na binafsi zitawawezesha kujadili viashiria vinavyo chochea Vitendo vya Rushwa.

Kupitia kusanyiko hilo litakalo fanyika kwa Siku mbili mfululizo litawawezesha kuwa wawazi katika mijadala na kuandaa Mikakati inayotekelezeka ili kuweza kugundua na kubainisha maeneo yanayotekeleza Vitendo vya Rushwa na kuchukua hatua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini Geita Gold Mine Limited (GGML), Duran Archery amesema kuwa kupitia Mkutano huo uliojumuisha Wadau mbali mbali na Watumishi wa Taasisi yake itawawezesha kushirikiana pamoja na kuwa na Mikakati ya pamoja ya kujenga Jamii yenye Maadili, Haki na Maendeleo ili kuweza kuwa na Jamii inayoishi kwa kuwa na Maadili ili kuweza kuleta Maendeleo.

Ameongeza kuwa Mkutano huo wa Siku mbili itawezesha Wadau hao kuwa na Mjadala na kuandaa Mikakati inayotekelezeka na pia utasaidia taratibu za utendaji, maombi ya zabuni mbali mbali katika Mgodi huo.

Naye Wakili Msomi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Denis Nyakayo amesema kuwa watahakikisha wanaendesha majukumu yao bila kuwepo viashiria vya Rushwa na kuimarisha Mikakati ya uadilifu Mahala pa Kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *