Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshiriki kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Siku mbili wa Maafisa Watendaji Wakuu wa Africa ulioanza hii leo Mei 12, 2025, jijini Abidjan nchini Ivory Coast.
Katika Mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo, ambao umefunguliwa na Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara umewakutanisha Maafisa Watendaji Wakuu zaidi ya 3,000, wawekezaji na Wakuu wa Nchi na Serikali.





