SERIKALI YAWAINUA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA VIUNGO

Serikali Nchini, kupitia Wizara ya Elimu imenunua na kusambaza vitimwendo 120, kompyuta 35, vishikwambi 45 na vinasa sauti vya kidigiti 48 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari 120 katika Halmashauri ambazo zilibainika kuwa na wanafunzi wengi wenye ulemavu wa viungo.

Akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati akiwasilisha Bungeni Mqkadirio na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2025-2026 ambapo amesema Serikali imenunua na kusambaza kompyuta mpakato, vitimwendo na vinasa sauti kwa wanafunzi 691 wanaosoma shule ya nyumbani katika shule 136 za msingi zilizobainika kuwa na upungufu wa vifaa.

Amesena Serikali imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kutoa elimu jumuishi kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapata vifaa na mahitaji yanayowawezesha kujifunza kwa ufanisi. Katika kufikia lengo hilo.

Hata hivyo amesema katika mwaka wa fedha 2025/26, Serikali kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia imepanga kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji wa elimu na mafunzo, kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa mafunzo ya amali katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Vilevile kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari na
ualimu, kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu, kuimarisha uwezo wa nchi katika utafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifuili kuchangia upatikanaji wa maendeleo endelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *