DC LULANDALA AWAPA SALAAM ZA PASAKA WANANCHI SIMANJIRO

Na Afarah Suleiman, Simanjiro – Manyara.

Mkuu wa wilaya Simanjiro, Fakii Lulandala ,leo April 19, 2025 amewatakia kheri ya pasaka wakristo wote wilayani Simanjiro na kuwata waadhimishe siku hiyo kwa upendo na amani.

Lulandala amewahimiza waumini na wananchi kwa ujumla kuendelea kulinda, kutunza na kudumisha amani ya nchi, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo na ustawi wa jamii.

Aidha Lulandala amewataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na utulivu kwenye nyumba za ibada hasa katika kipindi hiki Taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwisho mwa mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *