Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea na kukagua ujenzi wa Miradi ya Majisafi katika Kata ya Nala na Nkuhungu ili kuona maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo.
Katika ziara hiyo Waziri wa Maji ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.

Aweso ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingiria Dodoma(DUWASA), Mhandisi Aron Joseph kukamilisha mradi wa Nala katika kipindi cha Wiki mbili na kuhakikisha wananchi wanaanza kutumia Maji hayo.
Mradi huo wenye gharama ya shilingi bilioni 3.83 na kukamilika kwa asilimia 100 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.

Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huu kutanufaisha wakaziwapatao 5,188 wa Nala Centre, Segu Juu na Chihoni ndani ya Kata ya Nala pamoja na kiwanda cha mbolea cha Nala – Itracom.
Kutekelezwa kwa awamu ya pili ya mradi huu kutaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi wapatao 8,647.