STAKABADHI GHALANI IMESAIDIA KUONGEZA BEI KOROSHO – MAKALLA

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni msingi utakaowasaidia kwa wakulima kupata bei nzuri ya korosho, hivyo kimewataka wananchi wapuuze uongo unasemwa kuwa wakulima wananyonywa kwenye zao la korosho.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameeleza hayo leo Aprili 15,2025 katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, ikiwa ni miendelezo wa ziara yake ya siku 10 katika Mkoa wa Lindi na Mtwara.

Amesema kuwa hapo awali bei ya korosho ilishuka sana lakini kupitia mfumo huo wa stakabadhi ghalani maisha ya watu yamebadilika, hivyo anayetaka kuzungumza kuhusu korosho ajipange ili awe na hoja za kutosha kuzungumzia hilo.

“Leo hii mnauza korosho mpaka Sh 4000 kutoka bei ya chini zmya zamani alafu anakuja mtu anawaambia kwamba mnanyonywa nataka niwambie kwanza wale waliokuja hakuna aliyewahi kulima korosho wala anayejua uchungu wa kulima, hawajui hata ushirika,” amesema Makalla.

Ameongeza kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umefanya mapinduzi makubwa kwa kupeleka pembejeo na ruzuku lengo likiwa ni kuwasaidia wakulima na wapinzani wamekuwa ni sehemu ya wanufaika wa mapinduzi hayo yaliyofanywa na Rais Samia.

Makalla amesema Mafanikio hayo yamepatikana kutokana na uimara wa ushirika kwa kuuza korosho kwenye stakabadhi ghalani ambayo ni sera ya CCM kusaidia wakulima kwa lengo la kuimarisha ushirika.

Pia amewataka wananchi washirikiane na viongozi kuimarisha ushirika na kusimamia stakabadhi ghalani kwani bei za mazao zitaendelea kupenda kukiwa na ushirika imara ikiwa watashiriana na kufata miongozo mizuri inayotolewa na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *