Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Sekta Binafsi Ina Mchango Mkubwa katika Kukuza Sekta ya Utalii hapa nchini katika Nyanja tofauti na kusisitiza Serikali Kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi Ili kuwa na Utalii Endelevu.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipoifunga ziara Maalumu ya Mabalozi (Safari Diplomatic Tour) wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini iliolenga kuutangaza Utalii wa Tanzania na diplomasia ya Kiuchumi katika Nchi zao iliofanyika Hoteli ya Kwanza Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema, Serikali inaendelea kuchukua hatua Madhubuti za Kuimarisha Sekta ya Utalii Ili kuwa Endelevu na kuifanya Zanzibar kuwa Kituo Muhimu cha Utalii kinachotambulika na kuvutia Ulimwenguni huku akidai kuwa Utalii ni Sekta Muhimu na nguzo ya Uchumi wa Zanzibar ambayo mbali na Kukuza Uchumi Sekta Hiyo Inawaunganisha Watu wa Mataifa mbalimbali Ulimwenguni.
Dkt. Mwinyi amesema Serikali imechukua Juhudi kubwa za Uimarishaji wa Viwanja vya Ndege kwa lengo la kutoa huduma Bora kwa Watalii ,Upanuzi wa Miundombinu ya Barabara pamoja na Huduma za Afya,Umeme na Upatikanaji wa Maji ni hatua Muhimu za kufanikisha kuwa na Utalii unaovutia na Endelevu.

Aidha, amebainisha kuwa kuchukuliwa kwa hatua hizo kumefanya Nchi kupokea idadi kubwa ya Watalii kila Mwaka wanaofikia takribani Milioni mbili na kuiunganisha Zanzibar na Mashirika ya Kimataifa ya Ndege 34 yanayoleta Watalii hapa nchini.
Rais Dkt. Mwinyi pia amesema mikakati ya Uwekezaji imewezesha kupokea Watalii 548,503 Mwaka 2022 na Mwaka 2023 imepokea Wageni 736,755 na kutunukiwa Tuzo ya World Travel Award kwa kuwa Kituo kinachoongoza kwa Matamasha na Mikusanyiko ya kimataifa.