Na Frank Aman – Geita.
Ili kuweza kuleta Mabadiliko chanya katika Maisha ya Wanafunzi na Jamii kwa ujumla, Wahitimu wa ngazi mbali za Elimu ikiwemo Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu wametakiwa kutumia Elimu waliyoipata kutoka katika Taasisi mbali mbali za Elimu katika kuleta Mabadiliko mara baada ya kuhitimu Masomo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Geita ambaye pia ni Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Kata ya Kalangalala, Richard Nzagamba wakati wa Mahafali ya Wanafunzi wanaohitimu Elimu ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Mwatulole, ambapo amewahimiza Wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule hiyo kutumia vyema Elimu waliyoipata kwa manufaa na maendeleo ya Jamii.
Nzagamba alitoa wito huo wakati akimwakilisha, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Geita, Magambo Nkilosubi katika Mahafari ya Tano ya Kidato cha Sita yaliyofanyika Shuleni hapo.
Amesema ni muhimu kwa Wahitimu hao kutumia Maarifa yao kwa malengo chanya ikiwemo kuchagua Vyuo Vikuu vitakavyo wawezesha kupata ujuzi utakao wasaidia kujiajiri badala ya kusubiria waajiriwe pekee.
One response to “WAHITIMU WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA ELIMU KULETA MABADILIKO”
Hii ni kweli itasaidia kuinua uchumi wa kuanzia katika ngazi ya familia jamii na taifa kwa ujumla