SHAHJAHAN: ALIUWA WATU 27 AKAACHILIWA HURU AKIAHIDI KUWA RAIA MWEMA

Moja kati ya taarifa zilizowahi kutikisa ulimwenguni ni lile tukio la Mzee mmoja wa Bangladesh, Shahjahan Bhuiyan ambaye mwaka 1991 alihukumiwa na Mahakama kifungo cha miaka 42 jela kwa kosa la kumuua mtu bila kukusudia na kisha kuachiliwa huru wiki moja baadaye.

Kilichoshangaza si mzee huyu kuachiliwa huru kwa kuuwa mtu mmoja, bali kuachiliwa baada ya kuwauwa wafungwa wengine 26 akiwa gerezani na kuzua gumzo kubwa nchini humo na Ulimwenguni kiujumla, huku raia wengi wakitaka arudishwe tena gerezani la sivyo watajua la kufanya.

ILIKUWAJE:

Serikali kupitia Idara ya Magereza nchini humo, ilitangaza sababu za kumuachia huru Mzee huyo, ikisema alisaidia kazi ya kuwanyonga wafungwa hao 26, ambao walikuwa wamehukumiwa kunyongwa na Mahakama za nchini humo, kazi ambayo ilishindwa kutekelezwa na wahusika.

UTAYARI:

Iliarifiwa kuwa, Mzee huyo hakulazimishwa bali baada ya Idara ya Magereza kusema hakuna aliye tayari kuifanya kazi hiyo ya kuwanyonga wafungwa hao waliokaa muda mrefu, alijitolea kwa moyo mkunjufu na kupelekea kupata tena uhuru wake, kwa ahadi kuwa ataenda kuwa raia mwema kwa jamii.

Shahjahan Bhuiyan alipata umaarufu sana kwa tukio hilo, vitabu viliandikwa na vyombo vya Habari vingi vilimuhoji mara kwa mara.

Alizaliwa Machi 26, 1950 na huenda alionana tena na wale jamaa aliowanyonga Juni 24, 2024 alipoaga Dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Karibu sana kiiiweni, kuna Kahawa hapa, sema Kashata zimeisha, ila nakupa tahadhari kuwa makini na MAMBO YA NGOSWE, kule ni Bangladesh.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *