HALMASHAURI ZIANZISHE KLINIKI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIMU – DKT. BITEKO

Na Frank Aman – Geita.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Wakuu wa Wilaya kuanzisha Kliniki Maalumu inayolenga kusikiliza, kushughulikia na kutatua changamoto zinazo wakabili Walimu katika maeneo yao husika ili kuwezesha kupatikana kwa utatuzi wa Kero zao ambazo zimekuwa zikishusha Ari ya utendaji kazi kwa Watumishi hao na pia kuchangia kushuka kwa kiwango cha Elimu nchini.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa Kliniki ya kusikiliza na kutatua changamoto za Walimu Mkoani Geita ambapo amezitaka Taasisi za Serikali kuweka utaratibu Maalumu kutenga muda wao na kuanzisha Kliniki ndogo ndogo zinazolenga kusikiliza na kutatua Kero za Walimu kuanzia ngazi za  Wilaya na Mkoa walipo. 

Amesema, Kliniki ambayo itaweka kambi Mkoani hapa kwa zaidi ya Wiki mbili kuanzia Leo ina Lengo la kusikiliza kwa ukaribu Changamoto hizo zinazowakabili Walimu Mkoani hapa, ambapo Makamu wa Rais wa CWT, Seleman Ikomba ameeleza kuwa Kliniki hiyo imelenga katika kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Walimu hususani Masuala yahusuyo Madai ya malimbikizo ya malipo yao ya Likizo, Uhamisho na kupandishwa madaraja na masuala mengine yanayoihusu stahiki zao.  

Amesema kuwa Kliniki ya Samia ya kutatua Kero za Walimu kwa Mkoa wa Geita – _Teacher’s Mobile Clinic – Geita inaratibiwa na CWT kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Utumishi  na Utawala Bora, Ofisi ya Rais Tamisemi, Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Tume ya Utumishi wa Walimu ikiwa na Lengo kuu la kusikiliza na kutatua Kero za Walimu Mkoa wa Geita.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Joseph Misalaba amesema kupitia Kliniki hii itawakumbusha Walimu kutambua wahibu wao Kama nguzo ya Taifa kwa kujenga misingi imara ya  Watanzania kupitia Sekta ya Elimu Nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *