ACHENI MALUMBANO SHUGHULIKIENI MATATIZO YA WANANCHI – DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewasihi Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na watumishi wa serikali Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kujivunia hali ya kijografia ya Uchumi iliyopo Kahama na kushughulikia matatizo ya wanachi badala ya kulumbana wenyewe kwa weyewe na kukwamisha maen deleo.

Wito huo umetolewa Dkt. Biteko katika Mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Msalala uliolenga kupokea utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika kipindi cha mwaka 2020/25.

“Tusipotafsiri hali ya kijografia ya Kahama kiuchumi tukaaacha kuungana kwa pamoja kama wana Ccm tukashughulika maendeleo ya watu tukaanza kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe,wanachi watatushangaa kwani wao wanataka maendeleo hawataki Migogoro,” amesema Dkt.Biteko.

Aidha, ametoa wito kwa wana Kahama kumuombea Rais DR.Samia Hassan kwa juhudi za kupeleka maendeo kwa wanachi.

“Niwaombe Sana kazi moja mliyonayo tumuombee Rais wetu,Msalala kwa mfano ninyi mna utajiri mkubwa wa madini miaka yote mnaondolewa kama wachimbaji haramu,Mh Rasi amefanya uchimbaji wa madini ubaki mikononi mwenu,anahakikisha kila mahali walipo watanzia kuwe na Shule,Zahanati,Maji na vituo vya afya,” ameongeza Biteko.

Awali akiwasilisha utekelezaji wa ilani kwa jimbo la Msalala kwa mwaka 2020-2025 Mbunge wa jimbo la Msalala Alhaj Idd Kassimu Idd amewashukulu Watumishi wa halamshauri ya Msalala Pamoja na madiwani kwa ushirikiano wa Pamoja katika kufanikisha utekelezaji wa ilani.

“Mh Mgeni Rasmi niwapongeze Watumishi wote wa halmashauri ya Msalala Pamoja na waheshimiwa madiwani wote,Hawa unaowaona hapa ndiyo ambao mimi wakati natimiza majukumu yangu kuanzia mwaka 2020-2025 nilikuwa nao bega kwa bega katika kuhakikisha tunatekeleza vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi” Alisema Mbunge Idd.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amemshukuru naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko kwa kukubali kuja kuwanmgeni rasmi na amewasihi watumishi wote wa mkoa wa Shinyanga na wanachama wa ccm kwa ujumla kuzingatia umoja,Kushughulikia matatizo ya wanachi.

“Nikushukuru sana kwa kukubali wito huu,lakini pia niwaombe wana msalala tutoke hapa tukiwa wamoja,Twende tukashughulikie matatizo ya wananchi na tumalize tofauti zetu wate tuseme yaliyofanywa msalala,” alisema Macha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *