NETO HAINA USAJILI WA KISHERIA – RPC GEITA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limetoa Taarifa ya kushikiliwa kwa Joseph Paul, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alikamatwa February 24, 2025 kwa ajili ya mahojiano huku akijitambulisha kuwa yeye ni mhusika Mkuu wa Kundi Sogozi la Whatsapp la Umoja wa Walimu wasiokuwa na ajira nchini (NETO).

Jeshi la Polisi Geita limebaini kuwa hadi sasa uchunguzi wa awali umegundia kuwa umoja huo hauna usajili kutoka Mamlaka za Kisheria zinazoshughulika na usajili.

Tayari mtuhumiwa ameelezwa tuhuma dhidi yake na amehojiwa kwa mujibu wa Sheria na kupewa dhamana. 

Jeshi la Polisi inaendelea na uchunguzi na taarifa kamili itatolewa mara baada ya uchunguzi kukamilika na hatua za kisheria zitachukuliwa. Kamanda Jongo amewasisitiza Waananchi kuzingatia Sheria na kujiepusha na makundi ya kiharifu kwani Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu yoyote atakayebainika kuhusika katika Vitendo vya kihalifu au kuhamasisha uvunjifu wa amani.Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *