UGONJWA USIOJULIKANA WAUWA ZAIDI YA 50 DRC

Takriban watu zaidi ya 50 wamefariki dunia kaskazini magharibi mwa Taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana

Taarifa hiyo, imetolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kupitia Mkurugenzi wake wa Huduma za Afya, Serge Ngalebato katika Hospitali ya Bikoro.

Amesema, mlipuko huo wa hivi karibuni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeanza Januari 21 na visa 419 vimerikodiwa vikiwemo vifo 53.

WHO Afrika inaeleza kuwa, mlipuko wa kwanza ulitokea katika mji wa Boloko, baada ya Watoto watatu kula popo na kufa katika kipindi cha saa 48 kwa kupata homa kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *