SAKATA LA NETO: JOSEPH AACHIWA KWA DHAMANA GEITA

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limethibitisha kumkamata Mtuhumiwa na Kiongozi wa (NETO) Joseph Poul (31) Mkazi wa Geita kwa tuhuma za kuendesha Umoja wa kundi la Sogozi la watsup Moja ya kundi la walimu wasiokuwa na Ajira.

Akizungumzia Sakata hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita , SACP, Safia Jongo amethibitisha kumkamata kijana huyo February 24 , 2025 ambapo ameachiwa kwa dhamana huku chanzo cha awali kikidaiwa kuendesha umoja huo bila usajili.

“Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linathibitisha kumkamata mtuhumiwa aitwaye Joseph Poul (31) Mkazi wa Geita tarehe 24 mwezi wa pili 2025 kwa ajili ya mahojiano kuhusu akijitambulisha kuwa ni mhusika wa kundi Sogozi la Watsapp Mmoja wa Walimu wasio kuwa na ajira ,” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP, Safia Jongo.

“Hadi sasa uchunguzi wa awali ulibaini umoja huo hauna usajili wa aina yoyote mtuhumiwa ame hojiwa na ameshapewa dhamana Jeshi la polisi linaonya kutoa taarifa zaidi juu ya uchunguzi wa swala hilo kwa sababu uchunguzi bado unaendelea na watuhumiwa wengine bado hawajakamatwa , ” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP. Safia Jongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *