MATAMKO HAYAMALIZI VITA MJIKITE KWENYE UTENDAJI – KARDINALI AMBONGO

Kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kardinali Fridolin Ambongo ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwa na ujasiri wa kwenda mbali zaidi ya matamko, ili kupata suluhu ya mzozo wa Mashariki mwa DRC.

Wito wa Kardinali Ambongo unakuja ikiwa imepita siku chache tangu kufanyika kwa mkutano wa pamoja wa Viongozi kutoka Jumuiya za SADC na EAC.

WAKATI HUOHUO: Mamia ya watu wamejitokeza huko Brussels Ubelgiji kuandamana kuiunga mkono DRC na kuutuhumu Umoja wa Ulaya kutochukua hatua zozote, mandamano yanayokuja baada ya Viongozi wa SADC na EAC kujadili amani ya DRC.

Waandamanaji hao wamesema kutishwa vita haitoshi, inabidi kufuatilia kwa karibu utekelezwaji wa usitishwaji huo maana wanaopoteza maisha asilimia kubwa ni binadamu wasiokuwa na hatia yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *