Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji Willy Essomba Onana (23) raia wa Cameroon kutokea timu ya Rayon Sports ya Rwanda.
Onana amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC na ana uwezo wa kucheza namba zaidi ya tatu uwanjani, winga zote mbili na kucheza nyuma ya mshambuliaji namba 10.
Msimu uliopita Onana aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda akiwa na magoli 16 na assist 5 lakini ni Mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa Msimu nchini Rwanda yaani MVP.