Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Israel Imekiri Kumuua Kiongozi Mpya Wa Kundi La Hamas, Yahya Sinwar.

Chanzo: Dw

Israel imethibitisha kwamba vikosi vyake vimemuua kiongozi mpya wa kundi la Hamas, Yahya Sinwar, kufuatia operesheni yake katika ukanda wa gaza.

Wizara ya mambo ya nje ya Israel imethibitisha kifo cha kiongozi huyo wa Hamas aliyekuwa akisakwa, baada ya taarifa za awali za kufariki dunia kwa kiongozi huyo kusambaa.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuuawa kwa kiongozi huyo sio mwisho wa vita katika eneo hilo bali ni mwanzo wa mwisho na fursa kwa wakazi wa gaza kujikomboa kutoka utawala dhalimu wa wanamgambo.

Sinwar, anachukuliwa kama Mratibu Mkuu wa shambulio la oktoba 07, 2023 dhidi ya Israel ambalo lilisababisha vifo vya watu takribani 1,200 huku mamia wengine wakichukuliwa mateka.

Sinwar, alichukua wadhifa wa kiongozi wa kundi la Hamas
kufuatia kuuawa kwa Ismail Haniyeh huko Tehran, Iran mwezi Agosti mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *