Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kim Kardashian ahimiza kuachiliwa huru kwa Erik na Lyle Menendez

Mfanya Biashara Kim Kardashian ahimiza kuachiliwa huru kwa Erik na Lyle Menendez maarufu kama Menendez Brothers ambao walipatikana na hatia mwaka 1996 kwa kosa la mauaji ya wazazi wao.

Katika insha yake ya NBC News ameelezea historia ya ndugu hao ya unyanyasaji mkali na mabadiliko ya maisha yao mara baada ya kufungwa, na kwa maneno machache ameandika “tuna deni kwa wale wavulana wadogo waliopoteza utoto wao”

Sasa swali ni je Unawafahamu hawa Menendez Brothers??
Kama hauwafahamu basi leo acha nikupe kisa hichi cha kusikitisha kilichotokea miaka 35 iliyopita ambacho mpaka sasa kinafatiliwa na maelfu ya watu Duniani kote.

Joseph Lyle Menendez na Erik Galen Menendez ni ndugu wa Marekani ambao walihukumiwa mwaka 1996 kwa kosa la mauaji ya wazazi wao José Menendez ambaye alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Artisan Entertainment na mama yao Mary Louise.

Katika mahojiano yaliyofanywa mwaka 1996 mwezi wa sita na Barbara Walters, Menendez Brothers walielezea unyanyasaji wa kingono waliofanyiwa na baba yao mzazi Bw. Jośe Menendez wakati walipo kuwa wadogo na kwamba wamekuwa wakiishi maisha ya maumivu kutokan na unyanyasaji huo.

Menendez Brothers walisema kuwa waliumizwa zaidi na kitendo cha mama yao kuwa upande wa baba yao pamoja na kwamba walitumia njia zote kuelezea ukatili waliokuwa wakifanyiwa na baba yao.

Wapo mashahidi tofauti waliothibitisha kuwa ni kweli Bw Jośe alikuwa akiwafanyia ukatili watoto wake na mama yao Mary alikuwa haamini anachoambiwa na watoto wao.

Binamu yao Menendez, Diane Molen ambaye ni mtoto wa dada yake na Mary (mama wa Menendez) alitoa ushahidi wake na kusema kuwa mwaka 1976 aliishi na Familia Menendez na baada ya siku kadhaa Lyle Menendez alimwambia Diane kuwa amekuwa akifanyiwa unyanyasaji wa kingono na baba yake mzazi.

Diane aliamua kumwambia Mary ambaye ni mama yao na Menendez lakini haikuletq matokea chanya kwani mama yao alisimama upande wa baba yao.

Dada mkubwa wa Mama yao Menendez Bi. Joan Vander Molen pia aliunga mkono madai ya unyanyasaji wa kijinsia katika mahojiano ya 2017 na kituo cha habari cha People.

Baada ya kuishi katika manyanyaso ya kingono kwa muda mrefu ndipo Siku ya tarehe 20 mwezi wa nane mwaka 1989 wakati wa jioni Joseph lyle Menendez na Erik Galen Menendez kwa pamoja waliwaua wazazi wao Jośe Enrique Menendez na Mary louise kwa kuwapiga risasi.

Mpaka sasa wapo wanaosema kwamba ndugu hawa wameonewa na wapo waliochukizwa na walichokifanya huku wakiwaita mashetani.

Zipo Makala tofauti zilizowahi kusimulia kisa hichi ikiwemo Menendezi blood brothers 2017 na Monsters: The lyle and Erik Menendez story iliyotoka mwaka huu septemba 19, katika makala hii wameelezea namna walivyofanya mauaji hayo na maisha yao wakiwa gerezani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *