Mwanamke mmoja Mkoani Geita akatwa viganja vya mikono yake na watu wasiojulikana

Mwanamke Mmoja aliyefahamika kwa jina la Rehema Poul Mwenye umri wa miaka 26 Mkazi wa kitongoji cha Kapera kata ya Igulwa wilaya ya Bukombe Mkoani Geita amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mikononi hali iliyopelekea kupoteza viganja vyake vyote viwili vya mikono nakubakia mlemavu.

Akielezea kwa tabu namna alivyotendewa tukio hilo Rehema amesema alifanyiwa tukio hilo majira ya saa mbili usiku julai 25 mwaka huu wakati akitoka sokoni kuelekea nyumbani kwake baada ya kukutana na watu waliomjeruhi kwa kumkata vianganja na kuvitenganisha na mikono.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dr Gaudensia Mkapa amekiri kumpokea mwanamke huyo akiwa hajitambui na alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kwa kukatwa viganja vyake ambayo vimehifadhiwa mochwari kwa ajili ya kuwakabidhi ndugu zake na mwanamke huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Igulwa Lucy Ndile amesema alipata taarifa za tukio kutoka wananchi na baada ya kufika eneo husika alimkuta mwanamke huyo akiwa bado hajapelekwa hospitali ndipo alipotoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani humo na kumkimbiza hospitali haraka.

Nao baadhi ya mashuduha wa taukio hilo wamesekitishwa na kitendo alichofanyiwa mwananke huyo huku wakiliomba jeshi la polisi kuhakikisha linawasaka wahusika watuki hilo ili waweze kuchukulia hatua kali kwa lengo la kukomesha matukio kama hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *